Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ameahidi kukabiliana na Korea Kaskazini
Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ameahidi kukabiliana vilivyo na Korea Kaskazini baada ya matokeo ya kwanza kuonyesha kuwa alipata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi wa siku ya Jumapili. Bw. Abe alikuwa ameitisha uchaguzi wa mapema kwa ahadi ya kukabiliana na changamoto zinazoikabili Japan, likiwemo tisho kutoka Korea Kaskazini. Vyombo vya habari vinaripoti kuwa muungano wa Bw. Abe umeshinda theluthi mbili ya viti vya bunge. Hii inampa Bw. Abe nafasi ya kuifanyia mabadiliko katiba ya baada ya vita vya pili vya dunia. Awali waziri mkuu alikuwa ametoa wito wa kutaka jeshi la nchi lifanyiwe mabadiliko, hatua yenye utata ambayo anasema kuwa inahitajika kuboresha ulinzi wa jeshi la Japan. Akizungumza baada ya kutolewa matokeo ya kwaza Bw. Abe alisema: "Jinsi nilivyoahidi lengo langu kubwa ni kuikabili Korea Kaskazini. Vyombo vya habari vinaripoti kuwa muungano wa Bw. Abe umeshinda theluthi mbili ya viti vya bune. Miezi miwili tu iliyopita umaarufu wake ulikuwa ukishuka kufuatia kup...